Pata taarifa kuu
COLOMBIA-MAANDAMANO-SIASA-USALAMA

Raia waendelea kuandamana dhidi ya Rais Duque nchini Colombia

Raia wameandamana wakati wa mgomo wa kitaifa ulioitishwa na wanafunzi, vyama vya wafanyakazi na watu asilia nchini Colombia dhidi ya Rais wa nchi hiyo Ivan Duque, Bogota Novemba 21, 2019.
Raia wameandamana wakati wa mgomo wa kitaifa ulioitishwa na wanafunzi, vyama vya wafanyakazi na watu asilia nchini Colombia dhidi ya Rais wa nchi hiyo Ivan Duque, Bogota Novemba 21, 2019. © Raul ARBOLEDA / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Colombia imeendelea kukumbwa na mfululizo wa maandamano kupinga utawala wa rais wa nchi hiyo. Mamia ya maelfu ya Wakolombia walimiminika mitaani Alhamisi wiki hii katika maandamano yasiyokuwa ya kawaida dhidi ya Rais Ivan Duque, ambaye yuko madarakani kwa kipindi kisichozidi miezi 18.

Matangazo ya kibiashara

Katika mgomo na maandamano, vilivyoitishwa na vyama vya wafanyakazi, wanafunzi, watu asilia wa nchi hiyo, mashirika yanayotetea mazingira na upinzaji walijiunga na wenzao, wakishutumu sera za serikali ya mrengo wa kulia.

"Colombia imeshinda katika siku hii ya kihistoria ya maandamano ya kiraia," kamati inayosimamia mgomo katika ngazi ya kitaifa imebaini katika taarifa. Kamati hiyo inaundwa na mashirika yalioomba mkutano "wa haraka" na rais Ivan Duque na kuwatolea wito "raia kuwa tayari kuchukua hatua zaidi mitaani ikiwa serikali itaendelea kupuuzia madai ya waandamanaji".

Alhamisi jioni, rais Ivan Duque amesema kuwa amesikia madaia ya waandamanaji, lakini hakujibu kuhusu ombi la mazungumzo ya moja kwa moja.

"Leo, Wakolombia wameongea, tumewasikia, mazungumzo ya kijamii ni jambo muhimu kwa serikali hii. Tunapaswa kujadili kwa kina na wadau wote wa nchi," rais wa colombia amesema.-

Maandamano haya yanafanyika katika hali ya wasiwasi katika ukanda wa Amerika ya Kusini, ikiwa ni pamoja na machafuko ya kijamii na kisiasa, yaliyoibuka nchini Ecuador, kisha Chile na Bolivia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.