MAREKANI-MAUAJI-USALAMA

Wawili wauawa kwa kupigwa risasi Pearl Harbor, Marekani

Makumbusho ya Pearl Harbor.
Makumbusho ya Pearl Harbor. Wikipedia

Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi katika kambi ya jeshi la wanamaji ya Pearl Harbor, katika Kisiwa cha Hawaii, kinachopatikana kwenye Bahari ya Pasific.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo limetokea Jumatano Alfajiri, Desemba 4, viongozi wa jeshi katika eneo hilo wametangaza. Mshambuliaji aliyejihami kwa bunduki alijiua, baada ya kutekeleza mauaji hayo ya watu wawili.

"Mshambuliaji ametambuliwa kama askari wa jeshi la majini la Marekani," uongozi wa jeshi la majini limesema katika taarifa. "Alifyatua risasi na kujeruhi wafanyakazi wa kiraia wa Wizara ya Ulinzi kabla ya kujiua," kimesema chanzo hicho, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu sababu za mshambuliaji huyo.

Dakika chache baadaye, Mkuu wa jeshi la wanamaji Robert Chadwick alitangaza kwamba wafanyakazi wawili wa kiraia waliopigwa risasi wamefariki dunia kutokana na majeraha walioyapata. Mtu wa tatu bado anaendelea kupata huduma hospitalini, ameongeza Robert Chadwick.

Tukio hilo linakuja siku tatu kabla ya maadhimisho ya miaka 78 ya shambulio la Japan kwenye bandari ya kkisiwa hicho cha Hawaii, na kusababisha Marekani kuingia katika vita mnamo mwaka 1941.