MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Kesi ya ung'atuzi dhidi ya Trump: Trump akabiliwa na mashtitaka mawili

Wabunge kutoka chama cha Democratic nchini Marekani wametangaza mashtaka yanayomkabiliwa rais wa Marekani ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka na kulizuwia bunge kufanya kazi zake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya uchunguzi Adam Schiff na Spika wa Bunge Nancy Pelosi na Jerry Nadler.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya uchunguzi Adam Schiff na Spika wa Bunge Nancy Pelosi na Jerry Nadler. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Baraza la Wawakilishi litapiga kura katika kikao cha wiki ijayo.

Katika mkutano na waandishi wa habari, chama cha Democratic kimeweka wazi vipengele viwili vya mashitaka dhidi ya Rais Donald Trump ambavyo huenda vikamtia hatiani kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Akitangaza vipengele hivyo, Seneta Jerrold Nadler wa kamati ya sheria amesema wana ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani Rais Trump na kwamba hawatampa nafasi ya kuendelea kuvunja katiba ya taifa hilo kubwa duniani.

Bwana Trump anashutumiwa kwa kuzuia misaada kwenda kwa Ukraine kwa ajili ya manufaa yake ya kisiasa ndani ya Marekani.

Hata hivyo, Trump amepuuzia hatua hiyo na kuiona kama kampeni chafu dhidi yake.

Taarifa hiyo iliowasilishwa na bunge la wawakilishi itasababisha kufanyika kwa kura ya kumtoa madarakani.

Hatua hii ya kumuondoa madarakani ilianzishwa baada ya mtu ambaye hakutaka kujulikana kulalamika kwa bunge la Congress mwezi Septemba kuhusu simu iliyopigwa na rais Trump kwa rais wa Ukraine.

Mashitaka yaliyowekwa hadharani leo yanatokana na shinikizo la Trump kwa serikali ya Ukraine, akiitaka ianzishe uchunguzi dhidi ya wapinzani wake wa kisiasa, wakati akizuwia msaada kwa nchi hiyo.

Chama cha Democratic kinasema Bw Trump alitoa misaada miwili ya kijeshi yenye thamani ya dola milioni 400 za kimarekani ambazo tayari zilikuwa zimeshapangwa na bunge, na mkutano na rais Volodymyr Zelensky.

Chama cha Democratic kinasema shinikizo hili kwa mshirika wa Marekani linaonesha matumizi mabaya ya madaraka.

Hata hivyo, Trump amepuuzia hatua hiyo na kuiona kama kampeni chafu dhidi yake.