Pata taarifa kuu
CHILE-AJALI

Ndege ya kijeshi ya Chile yatoweka na watu 38

Rais wa chle Sebastian Pinera ambaye amesemaameandika katika ujumbe wa Twitter kwamba amesikitishwa na kutoweka kwa ndege ya kijeshi ya Chile ikiwa na watu 38
Rais wa chle Sebastian Pinera ambaye amesemaameandika katika ujumbe wa Twitter kwamba amesikitishwa na kutoweka kwa ndege ya kijeshi ya Chile ikiwa na watu 38 AFP Photos/Chilean Presidency/HO
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Ndege ya kijeshi ya Chile yenye chapa C-130 Hercules iliokuwa ikiabiri watu 38 imetoweka, kulingana na taarifa ya jeshi la wanaanga nchini humo. Kitengo cha habari cha EFE kimeripoti kwamba watatu kati ya abiria hao ni raia.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la anga la Chile linasema operesheni ya kutafuta sambamba na zoezi la uokoaji vinaendelea ili kuokoa ndege hiyo pamoja na watu ilioabiri.

Ndege mbili za kivita na meli nne zimetumwa kusaidia katika zoezi la kutafuta wa ndege hiyo.

Ndege hiyo ilitoweka baada ya kupaa kutoka mji wa Kusini wa Punta Arenas ikielekea Antarctica saa kumi na mbili (saa za Chile).

Wafanyakazi 17 na abiria 21 ambao walikuwa wakisafiri ili kutoa usaidizi wa kimipango ni miongoni mwa waliotoweka na ndege hiyo.

“Ndege hiyo haikuonyesha ishara zozote za kukabiliwa na tatizo kabla ya kutoweka, “ Mkuu wa jeshi la wanaanga nchini Chile Eduardo Mosqueira ameambia chombo cha habari.

Jenerali Eduardo Mosqueira anaamini kwamba ndege hiyo huenda ililazimika kutua baada ya kukabiliwa na upungufu wa mafuta katika safari yake ya kuelekea katika kambi ya rais wa Chile Eduardo Frei Montalya katika kiswa cha King George.

Wakati huo huo Rais wa Chile Sebastian Pinera ameandika katika ujumbe wa Twitter kwamba amesikitishwa na kutoweka kwa ndege hiyo huku akibaini kwamba anachunguza hali katika kambi ya kikosi ch awanaanga cha Cerrillos katika mji mkuu wa Santiago.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.