MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Baraza la Wawakilishi lapiga kura ya dhidi ya Donald Trump

Rais Donald Trump wakati akiwasili Michigan, Desemba 18, 2019.
Rais Donald Trump wakati akiwasili Michigan, Desemba 18, 2019. Brendan Smialowski / AFP

Baraza la Wawakilishi nchini Marekani limepiga kura dhidi ya Donald Trump kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia shughuli za bunge kwa kufanya uchunguzi dhidi yake.

Matangazo ya kibiashara

Kura hiyo ya kihistoria imepigwa Jumatano usiku. Baraza la Wawakilishi limemkuta na hatia ya kutumia vibaya madaraka na kuzuia uchunguzi wa Bunge. Donald Trump amekuwa rais wa tatu nchini Marekani kushtakiwa.

Baraza la Wawakilishi lilijadili kwa saa sita vifungu viwili vya mashtaka ya rais wa Marekani: matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia Bunge kufanya shughuli zake kuhusiana na uchunguzi dhidi yake. Bunge la Congress nchini Marekani linatawaliwa na chama cha Democratic.

Baraza la Wawakilishi limepitisha shutma hizo kwa, kura 230 dhidi ya 197 na moja ambayo haikutoa msimamo wowote.

Mchakato wa mwisho wa kura utalihusisha baraza la Seneti ambalo litakuwa na mamlaka ya kuamua kama anaweza kuondolewa madarakani au la.

Baraza la wawakilishi lina nguvu ya kumshitaki rais kwa wingi mdogo wa kura, lakini baraza la Seneti litahitaji wingi wa theluthi mbili kumuondoa rais madarakani, hatua ambayo sio rahisi kufanyika. Hii itakuwa ni mara ya tatu tu kwa rais wa Marekani kushitakiwa.