MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Kesi ya ung'atuzi dhidi ya Donald Trump kutatuliwa na Bunge la Seneti

Baada ya wabunge wa chama cha Democratic nchini Marekani kupiga kura ya kukosa imani na rais Donald Trump. Kwa sasa hatua inayofuata ni kuwa kesi hii itawasilishwa mbele ya Bunge la Seneti linalotawaliwa na chama chake Danald Trump cha Republican kuweza kutoa uamuzi iwapo ashtakiwe au la.

Kesi ya kumfungulia mashitaka Rais wa Marekani, Donald Trump kwa makosa "matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia shughuli za Bunge" yapelekwa mbele ya Bunge la Seneti.
Kesi ya kumfungulia mashitaka Rais wa Marekani, Donald Trump kwa makosa "matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia shughuli za Bunge" yapelekwa mbele ya Bunge la Seneti. MOHAMMED ABED / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wabunge wa chama Democratic ambao ni wengi katika bunge la wawakilishi, walichukua hatua hiyo baada ya kumtuhumu rais Trump kwa kulidharau bunge hilo la wawakilishi na kutumia vibaya madaraka yake.

Trump anakuwa rais wa tatu katika historia ya nchi hiyo kupigiwa kura ya kukosa imani na wabunge, lakini hakuna rais ambaye amewahi kuondolewa madarakani kupitia mchakato huo.

Baada ya hatua hiyo, Maseneta nao watapigia kura shutuma dhidi ya rais Trump mwezi Januari, na dalili zinaonesha kuwa, Trump atashinda kwa sababu, chama chake cha Republican kina idadi kubwa ya Maseneta.

Wanasiasa wa chama cha Democratic wanamshutumu rais Trump kwa kuishinikiza Ukraine kumchunguza mpinzani wake wa kisiasa, Makamu wa rais wa zamani Joe Biden.

Maseneta sasa wana kazi ya kupitia ushahidi kutoka kwa bunge la wawakilishi, na kuwasikiliza mashahidi na kuamua kwa kura iwapo rais Trump aondolewe madarakani au la.

Hata hivyo, haitakuwa rahisi kumwondoa madarakani rais Trump kwa sababu chama cha Republican kina Maseneta 53 huku kile cha Democratic kikiwa na Maseneta 45.

Ili kufanikiwa katika mpango wao, chama cha Democratic kinahitaji Maseneta 20 zaidi kutoka kwa Republican, suala ambalo halitakuwa rahisi.