MAREKANI-SHAMBULIZI-UGAIDI-USALAMA

Watu watano wajeruhiwa baada ya kuchomwa kisu nchini Marekani

Eneo ambalo shambulizi  lilitokea
Eneo ambalo shambulizi lilitokea REUTERS/Eduardo Munoz

Watu watano wamejeruhiwa baada ya kuchomwa kisu wakiwa ndani ya nyumba ya Rabbi katika jimbo la New York nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Polisi  wanasema shambulizi hilo lilitokea wakati watu wakisherehekea sikukuu ya Kiyahudi katika nyumba hiyo yenye wauamini wa Kiyahudi.

Ripoti zinasema kuwa, mmoja wa watu waliojeruhiwa, alichomwa kisu mara sita na baada ya tukio hili,  polisi wamesema wanaendelea kupiga doria katika makaazi ya waumini wa Kiyahudi kuhakikisha kuwa wanakuwa salama.

Maafisa wa usalama hata hivyo, walifanikiwa kumkamata mshukiwa na wanamzuia.

Gavana wa jimbo la New York Andrew Cuomo amelaani tukio hilo na kusema kuwa ameagiza uchunguzi kufanyika kubaini ukweli zaidi kuhusu kilichotokea.

Hata hivyo, Cuomo, ameelezea shambulizi hilo kama la kigaidi na kuongeza kuwa aliyetekeleza alilenga kuzua hofu miongoni mwa waumini wa Kiyahudi.

Hadi sasa lengo la shambulizi hili halijafahamika lakini uongozi wa jimbo hilo unaaminiwa kuwa umechochewa na chuki.