MAREKANI-KURA ZA MCHUJO-SIASA

Kura za mchujo Marekani: Bernie Sanders aibuka mshindi New Hampshire

Seneta Bernie Sanders amejiweka kwenye nafasi nzuri baada ya kyendelea kufanya vizuri katika kura za mchujo New Hampshire Februari 11, 2020.
Seneta Bernie Sanders amejiweka kwenye nafasi nzuri baada ya kyendelea kufanya vizuri katika kura za mchujo New Hampshire Februari 11, 2020. REUTERS/Rick Wilking

Seneta Bernie Sanders ameibuka mshindi katika Jimbo la New Hampshire katika kura za mchujo za kumtafuta mgombea atakayepeperusha bendera ya chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Bernie Sanders alipata ushindi huo akifuatiwa kwa karibu na Pete Buttigieg na Amy Klobuchar.

Alikuwa tayari alishinda katika kura za mchujo zilizopita huko New Hampshire, jimbo dogo lenye wakaazi milioni 1,3 linalopatikana Kaskazini Mashariki mwa Marekani, mwaka 2016.

Bernie Sanders anaonekana kama mshindi wa kura za mchujo kwa mara ya pili, akifuatiwa na Pete Buttigieg, ambaye aliibuka mshindi katika eneo la Iowa wiki iliyopita.

"Ushindi huu ni mwanzo wa kushindwa kwa Donald Trump," Bernie Sanders amesema.

Bernie Sanders na Pete Buttigieg sasa wamejiweka katika kundi la wagombea ambao wanatia kumuangusha Donald Trump katika uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.