PERU-UN-PEREZ-HAKI

Katibu Mkuu wa zamani wa UN Javier Perez de Cuellar afariki dunia

Javier Perez de Cuellar, Agosti 1988 wakati alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Javier Perez de Cuellar, Agosti 1988 wakati alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Mark CARDWELL / AFP

Javier Perez de Cuellar, mwanadiplomasia wa Peru na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 1982 na 1991, amefariki dunia Jumatano jioni Machi 4 huko Lima akiwa na umri wa miaka 100, mtoto wake ametangaza.

Matangazo ya kibiashara

"Baba yangu amefariki dunia saa 8:09:00 (sawa na 01:09 Alhamisi asubuhi, saa za kimataifa) na anapumzika kwa amani," amesema Francisco Perez de Cuellar, mtoto wa Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa kwenye redio ya serikali ya Peru, RPP Jumatano hii Machi 4 jioni.

Mwili wa mwanadiplomasia huyo wa zamani atapewa heshima za mwisho siku ya Ijumaa Machi 6 katika Jumba la Torre Tagle, makao makuu ya Wizara ya Mambo ya nje ya Peru, kabla ya kuzikwa katika makaburi ya Presbitero Maestro huko Lima.

Javier Perez de Cuellar alizaliwa Lima mwaka 1920, na alikuwa katibu mkuu wa tano wa Umoja wa Mataifa, ambaye alisherehekea siku yake ya kuzaliwa Januari 19, akitimiza umri wa miaka 100.

Nchini Peru, Javier Perez de Cuellar wakati huo alikuwa rais wa Baraza la Mawaziri na Waziri wa Mambo ya Nje wakati wa serikali ya mpito ya Valentin Paniagua, kuanzia Novemba 22, 2000 hadi Julai 28, 2001. Aliwahi kuwa mgombea wa urais katika uchaguzi wa mwaka 1995, lakini alipigwa mweleka na Alberto Fujimori, aliyechaguliwa kwa muhula mwingine.