MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Joe Biden aungana na Bernie Sanders baada ya kupata ushindi katika majimbo 4 kati ya 6

Joe Biden, mgombea wa chama cha Democratic katika kura za mchujo, na mkewe Jill Biden, huko Philadelphia Machi 10, 2020.
Joe Biden, mgombea wa chama cha Democratic katika kura za mchujo, na mkewe Jill Biden, huko Philadelphia Machi 10, 2020. MANDEL NGAN / AFP

Joe Biden amepata fursa ya kumuangusha mpinzani wake Bernie Sanders katika kura za mchujo zilizopigwa Jumanne wiki hii, katika kinyang'anyiro cha kumtafuta mgombea wa chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais wa Novemba mwaka huu nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Joe Biden ameamua kuungana na mpinzani wake Bernie Sanders akibaini kwamba ni mbinu mpya ya "kumshinda" Donald Trump.

"Pamoja tutamshinda" Donald Trump, amesema Joe Biden, makamo wa rais wa Barack Obama.

Joe Biden amepata ushindi mkubwa katika majimbo manne kati ya Sita, ikiwa ni pamoja na Mississippi, Missouri, Idaho, na haswa Michigan.

Matokeo bado hayajaruhusu mshindi katika eneo la Dakota Kaskazini na Jimbo la Washington.

"Nataka kumshukuru Bernie Sanders na wafuasi wake kwa nguvu na bidii yao isiyo ya kawaida," amesema Joe Biden.

"Lengo letu ni moja na kwa pamoja, tutamshinda Donald Trump, tutaunganisha nchi hii", ameongeza Joe Biden katika hotuba yake.