MAREKANI-MEXICO-CORONA-AFYA

Coronavirus: Marekani kutuma askari wake kwenye mpaka na Mexico

Utawala wa Trump una hofu kwamba ugonjwa wa Covid-19 husababisha zaidi wahamiaji haramu kujaribu kuingia nchini Marekani, mesema ofisa mmoja, ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Utawala wa Trump una hofu kwamba ugonjwa wa Covid-19 husababisha zaidi wahamiaji haramu kujaribu kuingia nchini Marekani, mesema ofisa mmoja, ambaye hakutaka jina lake litajwe. REUTERS

Pentagon itatuma askari wapatao 500 kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico kusaidia maafisa wa mipaka kuimarisha ulinzi wakati huu kunaripotiwa mgogoro wa kiafya kutokana na janga la Corona, shirika la habari la Reuters, limenukuu vyanzo vitatu kutoka Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Vyanzo hivi vimesema kwamba Pentagon iliidhinisha ombi lililotolewa na Idara ya Usalama wa Nchi.

Askari wapatao 5,000 tayari wanapiga kambi kwenye mpaka wa kusini mwa Marekani kusaidia maafisa wa mipaka kutekeleza majukumu yao ambayo hayahusiani na yale ya vikosi vya usalama.

Jumatatu wiki hii Mexico ilitangaza hali ya dharura ya kiafya na kuchukuwa hatua kali za kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19, ambapo zaidi ya watu elfu moja wameambukizwa ugonjwa virusi vya ugonjwa huo nchini.

Utawala wa Trump una hofu kwamba ugonjwa wa Covid-19 husababisha zaidi wahamiaji haramu kujaribu kuingia nchini Marekani, wakati ugonjwa huo unaathiri uchumi wa Mexico ambao umedorora, amesema ofisa mmoja, ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Wizara ya Usalama wa Nchi haijatoa maelezo zaidi kuhusu hali hiyo.