Pata taarifa kuu
MAREKANI-SANDERS-SIASA

Sanders ajiondoa katika kinyang'anyiro cha urais Marekani

Ni katika taarifa ambapo Bernie Sanders ametangaza kwamba amesitisha kampeni yake ya uchaguzi wa urais wa Marekani, Aprili 8, 2020.
Ni katika taarifa ambapo Bernie Sanders ametangaza kwamba amesitisha kampeni yake ya uchaguzi wa urais wa Marekani, Aprili 8, 2020. REUTERS/Lucas Jackson/File Photo
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Seneta Bernie Sanders amejiondoa katika kinyang'anyiro cha urais, huku akiahidi kushirikiana na Joe Biden, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kushinda katika kura za mchujo katika chama cha Democratic.

Matangazo ya kibiashara

Bw Sanders amewatolea wito wafuasi wa chama chake cha Democratic kushikamana vilivyo kwa kumshinda Donald Trump katika uchaguzi wa urais ambao umepangwa kufanyika mwezi Novemba.

Katika kuwatangazia wafuasi wake kwamba anajiondoa katika kura za mchujo za chama cha Democratic, Bernie Sanders amemsifu Joe Biden kama "mtu anayeheshimika sana" na kutangaza kwamba atashirikiana na mgombea mwenye msimamo wa wastani ili kuendeleza mpango wake uliozimwa na mrengo wa kushoto.

Baada ya kuelewa kuwa kuna mivutano kati ya kambi hizo mbili, Makamu wa zamani wa rais wa Marekani, Joe Biden, mwenye umri wa miaka 77, ameamua kuungana haraka na wafuasi wa Bernie Sanders mwenye umri wa miaka 78.

"Najua mtanipigia kura. Na najua inaweza kuchukua muda. Lakini nataka mjue kuwa ninawaona, ninawasikia, na kwamba ninaelewa kwa haraka mnachokitaka," amesema ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter Joe Biden, ambaye atachuana na Donald Trump Novemba 3, 2020.

"Natumai utajiunga nasi. Tunakuhitaji!", ameaongeza Bw Biden.

Licha ya kutambua kwamba "Joe Biden atakuwa mgombea mteule" wa chama cah Democratic ili kumuangusha Donald Trump katika uchaguzi wa urai, Bernie Sanders mwenye umri wa miaka 78 ametangaza kwamba ataendelea kuchuana katika kura za mchujo zilizosalia ili kukusanya wajumbe zaidi ambao watamruhusu "kutoa ushawishi mkubwa katika programu ya chama" wakati wa mkutano wa chama cha Democratic mwezi Agosti.

"Kwa pamoja, kwa kuungana, tutamshinda Donald Trump, rais hatari zaidi katika historia ya kisasa ya Marekani," ameongeza katika hotuba iliyorushwa mtandaoni kutoka nyumbani kwake Burlington, Vermont.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.