Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Rais wa Marekani Donald Trump atangaza mpango wa kuanza kurejea kwa hali ya kawaida

Hivi karibuni Rais wa Marekani Donald Trump awali amelishutumu shirika la Afya Duniani, WHO, kwa kuipendelea China.
Hivi karibuni Rais wa Marekani Donald Trump awali amelishutumu shirika la Afya Duniani, WHO, kwa kuipendelea China. AFP Photos/Getty Images North America/Alex Wong

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa mpango wa shughuli za kawaida kuanza kurejelewa hivi karibuni katika majimbo mbalimbali nchini humo wakati huu, idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona ikifikia zaidi ya Laki Sita na nusu, na idadi ya vifo ikifikia zaidi ya Elfu 32.

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni Rais Donald Trump alitangaza hali ya dharura kutokana na kuenea kwa virusi vya corona, pamoja na upatikanaji wa karibu dola bilioni 50 kama msaada zaidi wa serikali ya shirikisho kupambana na ugonjwa huo.

Trump amekabiliwa na ukosoaji kutoka kwa baadhi ya wataalamu juu ya hatua za kujivuta na zisizo na ufanisi katika kushughulikia janga hilo.

Athari za mripuko wa virusi vya corona katika maisha ya kila siku zimezidi kuongezeka duniani kote. Shule, biashara vimefungwa kwenye nchi kadhaa kujaribu kupunguza kuenea mripuko, huku pia sekta ya michezo nayo ikiathirika. Viongozi mbali wa dunia, nyota wa michezo na watu maarufu ni miongoni mwa maelfu ya watu walioambukizwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.