Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Karantini-Corona: Trump atoa wito wa "kukomboa" majimbo yanayotawaliwa na Democrats

Waandamanaji wakibebelea silaha huko Lansing, Michigan mnamo Aprili 15, 2020.
Waandamanaji wakibebelea silaha huko Lansing, Michigan mnamo Aprili 15, 2020. © AFP
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Rais wa Marekani Donald Trump ameonekana kuunga mkono vuguguvugu nchini humo linaloshinikiza  kuondolewa sharti la kutotoka nje lilowekwa kupambana na janga la Corona.

Matangazo ya kibiashara

Trump kwenye chapisho lake katika mtandao wa kijamii ametoa wito wa kurejea shughuli za kawaida katika baadhi ya majimbo yakiwemo Minnesota, Michigan na Viriginia, huu ukiwa msimamo tofauti na baadhi ya magavana wa majimbo hayo.

Majimbo haya matatu yanaongozwa na magavana kutoka chama cha Democratic ambao wameamuru wakaazi wao kukaa nyumbani.

Ugonjwa wa Covid-19 umesababisha vifo vya watu zaidi ya 30,000 nchini Marekani, ambapo hadi Ijumaa wiki hii kumekuwa kunaripotiwa visa 700,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona, kulingana na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

Watu karibu 2000 wamefariki dunia katika Jimbo la Michigan, 208 katika Jimbo la Virginia 208 na 87 katika Jimbo la Minnesota.

Katika majimbo haya, waandamanaji wiki hii walikiuka agizo la kukaa nyumbani ili kupinga hatua ya kukaa karantini na kutoa wito kwa magavana wa majimbo hayo kufungua shughuli za kuchumi.

Huko St Paul, katika Jimbo la Minnesota, mamia ya waandamanaji walikusanyika jana Ijumaa mbele ya makazi ya Gavana Tim Walz, huku wakisema "Minnesota yatakiwa kuwa huru", kulingana na vyombo vya habari vya katika jimbo jilo.

Huko Lansing, mji mkuu wa Michigan, waandamanaji 3,000 ambao baadhi yao walikuwa wakibebelea silaha Jumatano wiki hii waliandamana, huku wengine wakibeba mabango yanayomsifu Donald Trump. Hata hivyo Gavana Gretchen Whitmer amelaani kitendo hicho cha kubebelea silaha wakati wakiandamana.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.