Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA-UHAMIAJI

Covid-19: Trump atangaza kusitishwa kwa muda zoezi la kuwapokea wahamiaji

Donald Trump wakati wa mkutano wa kila siku na waandishi wa habari kuhusu janga la Corona, katika Ikulu ya White, Aprili 20, 2020.
Donald Trump wakati wa mkutano wa kila siku na waandishi wa habari kuhusu janga la Corona, katika Ikulu ya White, Aprili 20, 2020. REUTERS/Jonathan Ernst
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Kufuatia mgogoro wa kiuchumi uliyosababishwa na janga la Covid-19, Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kwamba anataka "kulinda ajira" za Wamarekani.

Matangazo ya kibiashara

"Kwa kuzingatia shambulio la adui asiyeonekana, na kutokana na haja ya kulinda ajira za raia wetu wakuu wa Marekani, nitasaini agizo la rais la kusitisha kwa muda zoezi la kupokea wahamiaji nchini Marekani, " Donald Trump ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Rais wa Marekani, ambaye katika kampeni yake ya uchaguzi alilisisitiza kwamba atasitisha zoezi la kuwapokea wahamiaji nchini Marekani, kama atafanikiwa kuwa rais wa nchi hiyo, hakutoa maelezo zaidi kuhusu jinsi gani anatarajia kutekeleza uamuzi huo na kwa muda gani.

Mapema mwezi wa Januari, alizuia safari zozote kwenda China ambapo virusi vya Corona vilianzia mwezi wa Desemba mwaka jana, kabla ya kupiga marufuku safari kati ya Marekani na nchi nyingi za Ulaya katikati mwa mwezi Machi.

Zaidi ya watu 42,000 wafariki dunia

Ugonjwa wa Covid-19, ambao Donald Trump anaiita "adui asiyeonekana", umewauwa zaidi ya watu 42,000 nchini Marekani, ambapo visa 766,660 vya maambukizi vimethibitishwa. Wamarekani milioni 22 pia wamepoteza ajira kutokana na mdororo wa kiuchumi uliosababishwa na janga hilo.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.