MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Trump akubali kuongeza idadi ya majaribio New York

Andrew Cuomo, Gacana wa mji wa New York.
Andrew Cuomo, Gacana wa mji wa New York. REUTERS/Mike Segar

Rais wa Marekani Donald Trump amekubali kwamba serikali ya shirikisho itasaidia mji wa New York kuongeza mara mbili uwezo wake wa kufanya vipimo vya ugonjwa naosababishwa na virusi vya Corona, Gavana wa jiji hilo Andrew Cuomo amesema.

Matangazo ya kibiashara

Kufuatia kupunguwa kwa idadi ya wagonjwa katika hospitali za huko New York, Cuomo aamesisitiza kuhusu umuhimu wa kufanya majaribio zaidi ya vipimo ili kuhakikisha wakazi wa mji wa New York wanarudi kazini.

Cuomo ametangaza kwamba New York inalenga kuongeza idadi ya watu wanaopimwa kila siku na kubaini kwamba zoezi hilo litachukua wiki kadhaa.

New York ndio kitovu cha ugonjwa huo nchini Marekani, ukiwa na visa 257,000 vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 ambao umesababisha vifo 20,000.