MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Trump kusaini sheria kuhusu uhamiaji

Rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump. REUTERS/Kevin Lamarque

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza Jumatano kwamba atasaini agizo la rais leo kuzuia wahamiaji kwa lengo la kuwalinda wafanyakazi wa Marekani katika muktadha wa mgogoro wa kiuchumi unaosababishwa na janga la Covid-19.

Matangazo ya kibiashara

Sheria hiyo itatumika kwa muda wa siku 60 kwa raia wa kigeni wanaotafuta "kadi ya kijani", cheti kinacho mruhusu raia wa kigeni kuishi na kufanya kazi kisheria nchini Marekani bila visa.

Lakini, raia wa kigeni waliopewa visa ya muda sheria hiyo hitowahusu. Watu hao ni pamoja na wafanykazi wa kigeni wanaotumika katika mashamba kwa msimu ambao wana jukumu muhimu katika uzalishaji na usambazaji wa chakula.

Mpango huo wa rais ulizua sintofahamu katika kambi ya Wademocrats, ambapo baadhi watuhumiwa Donald Trump kutaka kuepuka kukusolewa kuhusu jinsi alivyosimamia mgogoro wa Covid-19.

Wanasema kuwa kufungwa kwa mipaka na kusimamishwa kwa safari za ndege katika mapambano dhidi ya kuenea kwa virusi hivyo kumesababisha kumezuia wahamiaji kuingia nchini Marekani.