Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA-MAZUNGUMZO-CORONA

Coronavirus / Venezuela: Serikali na upinzani waanza mazungumzo ya siri

Serikali ya Kisoshalisti ya Venezuela na upinzani wameanza mazungumzo ya siri.
Serikali ya Kisoshalisti ya Venezuela na upinzani wameanza mazungumzo ya siri. REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Washirika wa Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro na wale wa mpinzani wake, kiongozi wa upinzani Juan Guaido, wameanza mazungumzo ya siri wakati hofu imetanda nchini Venezuela juu ya athari ya kuenea kwa virusi vya Corona, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya yanafanyika wakati kuna wasiwasi mkubwa kuhusu janga la COVID-19, mfumuko wa bei na uhaba wa mafuta na pia hofu kwa baadhi ya wafuasi wa Chama tawala cha Kisoshalisti ambao wana wasiwasi juu ya jinsi ya kuendelea na maisha yao ya kisiasa ikiwa kutakwa na mabadiliko katika serikali, wakati Washington imeendelea kuongeza vikwazo vyake.

Mazungumzo haya yanaonesha kuwa washirika wa Maduro na wale wa Guaido hawaamini kuwa kila upande unaweza kushinda mwingine katika muktadha wa janga la kimataifa na mpango mkubwa wa vikwazo vya Marekani vinavyolenga kumshinikiza Maduro aondoke madarakani.

"Kuna mambo mawili muhimu: Maduro na wale ambao wanaamini kwamba virusi vya Corona vitamaliza uongozi wa Guaido, na wale wa upande mwingine [ambao] wanatarajia kwamba mgogoro huo utamuangusha Maduro," amesema mwanasheria mmoja wa upinzani ambaye yuko tayari kwa maridhiano.

Hijajulikana ni lini mazungumzo hayo yalianza, wapi na jinsi gani yanafanyika, au upi mtazamo wa Maduro na Guaido kuhusu mazungumzo hayo. Vyanzo saba, vinavyowakilisha pande zote mbili hasimu katika siasa ya Venezuela, vimethibitisha mazungumzo haya.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.