Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Marekani yapitisha mpango wa kuokoa uchumi unaokabiliwa na Covid-19

Spika wa baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi amesema mpango huo ni muhimu kwa kuzilinda familia za Marekani na kuhakikisha kuwa kampuni ndogo ndogo zina rasilimali zinazohitaji.
Spika wa baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi amesema mpango huo ni muhimu kwa kuzilinda familia za Marekani na kuhakikisha kuwa kampuni ndogo ndogo zina rasilimali zinazohitaji. REUTERS/Tom Brenner
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Bunge la Congress limeidhinisha mpango mpya wa kuokoa uchumi wa Marekani dhidi ya janga la Covid-19 ambao umeuwa watu karibu Elfu 50 nchini.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya Bunge la Seneti, wajumbe wa Baraza la Congress wamepitisha kitita cha dola bilioni 483 (sawa na euro bilioni 450) kusaidia uchumi wa Mareakni ambao unakabiliwa na janga la Covid-19.

Mpango ambao bado unatarajiwa kutiliwa saini na Donald Trump, leo Ijumaa jioni.

Mpango huo unaongeza kwa ule wa trilioni 2.2 ulioidhinishwa mwishoni mwa Machi.

Idadi ya watu wlioambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani imefikia 866,646.

Spika wa baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi amesema mpango huo ni muhimu kwa kuzilinda familia za Marekani na kuhakikisha kuwa kampuni ndogo ndogo zina rasilimali zinazohitaji.

Wakati huo huo katika Ikulu ya Marekani, wanasayansi wamesema wamegundua kuwa kirusi hicho kinaharibiwa haraka na miale ya jua, na kutoa matumaini kuwa janga hilo litapungua wakati msimu wa joto ukianza.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.