MAREKANI-MONCEF-CORONA-AFYA

Coronavirus: Moncef Slaoui, Daktari anayetafuta chanjo ya Donald Trump

Rais Donald Trump akimsikiza Moncef Slaoui, mkuu wa zamani wa kitengo cha chanjo cha GlaxoSmithKlines, akizungumzia juu ya maendeleo ya chanjo ya coronavirus katika bustani ya White House Mei 15, 2020 huko Washington.
Rais Donald Trump akimsikiza Moncef Slaoui, mkuu wa zamani wa kitengo cha chanjo cha GlaxoSmithKlines, akizungumzia juu ya maendeleo ya chanjo ya coronavirus katika bustani ya White House Mei 15, 2020 huko Washington. Drew Angerer / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / Getty Images via AFP

Nchini Marekani, kama mahali pengine duniani, chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 inaendelea kutafutwa kwa udi na uvumba. Huko Washington, kazi hiyo imepewa Daktari Moncef Slaoui.

Matangazo ya kibiashara

Daktari huyo wa ugonjwa sugu wa saratani, ambaye ni raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Morocco ameteuliwa na rais wa Marekani Donald Trump na kuonyeshwa kwa vyombo vya habari kutoka ikulu ya White House.

Mbele ya waandishi wa habari, Donald Trump amemsifu Moncef Slaoui, ambaye amemteua kuiongoza timu inayo jukumu la kupata chanjo dhidi ya Covid-19 mwishoni mwa mwaka huu.

Kazi ngumu lakini itazaa matunda mazuri, amesema Moncef Slaoui: "Mheshimiwa rais, hivi majuzi niliona matokeo ya kwanza ya uchunguzi wa kliniki juu ya chanjo. Pamoja na data hizi, nina hakika zaidi kuwa tutaweza kutoa mamilioni milioni ya dawa ya chanjo ifikapo mwisho mwa mwaka wa 2020. "

Dk. Slaoui ambaye hana umaarufu sana, amejinyakulia sifa nyingi katika sekta ya chanjo.

Moncef Slaoui ambaye alizaliwa hukoAgadir, nchini Morocco, alisomea huko Brussels katika kitengo cha ugonjwa sugu wa saratani-chanjo na baiolojia. Kwanza alikuwa mwalimu nchini Ubelgiji, na baadaye alijiunga na maduka makubwa ya dawa na akachukuwa nafasi ya 2.

Mnamo mwaka wa 2016, Gazeti la Fortune lilimpa nafasi kati ya watu 50 wanaobadili ulimwengu. Moncef Slaoui ameshiriki hasa katika maendeleo ya chanjo dhidi ya gastroenteritis kwa watoto na saratani ya shingo ya kizazi.

Moncef Slaoui, 60, sasa anaishi kati ya Marekani na London. Hadi siku chache zilizopita, alikuwa sehemu ya kampuni inayosimamia masuala ya baiolojia na teknolojia ambayo imekuwa inafanya kazi kwenye chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Hata kama amesema kuwa kazi aliyopewa sio rahisi, Moncef Slaoui anahakikishia kwamba asingekubali kamwe ikiwa hakuwa na uhakika wa kufanikiwa.