Covid-19: Vifo vipya 1,255 vyathibitishwa nchini Marekani
Imechapishwa:
Marekani, nchi inayoendelea kuathirika zaidi na janga la Corona imerekodi visa vipya, 1,255 maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa vya Covid-19 ndani ya kipindi cha saa 24 zilizopita, kulingana na hesabu za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.
Jumla ya watu 94,661 wamefariki dunia kutokana na virusi vya Corona nchini Marekani nchini, kwa jumla ya visa 1,576,542 vya maambukizi vilivyothibitishwa.
Wakati huo huo visa vipya 25,582 vya maambukizi vimeripotiwa kati ya saa 8:30 usiku Jumatano na Alhamisi jioni).
Kumekuwa na wasiwasi nchini Marekani kuwa hivi karibuni, huenda idadi ya vifo itaongezeka na kufikia zaidi ya 100,000.
Hayo yanajiri wakati watu wengine 328,000 kote duniani wamepoteza maisha kutokana na virusi hivi ambavyo vimeendelea kuleta hali ya sintofahamu duniani.