Pata taarifa kuu
MAREKANI-CHINA-VIKWAZO-USHIRIKIANO

Marekani yaionya China kwa vikwazo zaidi

Uhusiano kati ya Marekani na China umeendelea kuzorota  kufuatia janga la Corona, ambalo Marekani inaamini limesababishwa na China.
Uhusiano kati ya Marekani na China umeendelea kuzorota  kufuatia janga la Corona, ambalo Marekani inaamini limesababishwa na China. Greg Baker / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Marekani imeonya China huenda ikawekewa vikwazo kufuatia sheria ya usalama inayopendekezwa kutekelezwa katika jimbo la  Hong Kong. Sio mara ya kwenza China kuwekewa vikwazo na Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati polisi wa jiji la Hong Kong wametumia gesi ya kutoa machozi na maji ya kuwasha ili kuwakabili maalfu ya waandamaji waliojitokeza kupinga mswada wa sheria kali juu ya usalama wa taifa uliopendekwa na China.

Wapinzani wa sharia hiyo wanasema inaenda kinyume cha kanuni ya nchi moja mifumo miwili, inayohakikisha uhuru wa jimbo la Hong Kong usiokuwapo China bara.

Makundi ya waandamanaji waliovaa nguo nyeusi walikusanyika ili kuupinga mswada huo wa sheria. Watu hao walitoa kauli mbiu za kusisitiza msimamo wa pamoja na ukombozi wa Hong Kong. Watu wapatao 120 walikamatwa na polisi kwa kujiunga na mikusanyiko isiyoruhusiwa.

Wakati huo huo Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani, Mike Pompeo, amesema sheria hiyo inaipa China uhuru wa kuitawala Hong Kong licha ya kutambuliwa kuwa  jimbo lenye madaraka na uhuru.

Uhusiano kati ya Marekani na China umeendelea kuzorota  kufuatia janga la Corona, ambalo Marekani inaamini limesababishwa na China.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.