Pata taarifa kuu
MAREKANI-HAKI ZA BINADAMU-MAUAJI

Marekani: Maafisa wanne wa polisi ya Minneapolis wachukuliwa hatua kali baada ya kifo cha raia mweusi

Maafisa wanne wa polisi katika eneo la Minneapolis nchini Marekani wamefutwa kazi baada ya mkanda wa video kuonesha mmoja wao akimkaba koo na goti lake raia mweusi, ambaye alifariki hospitalini Mei 26, 2020. Mtu ambaye hakuwa na silaha yoyote.
Maafisa wanne wa polisi katika eneo la Minneapolis nchini Marekani wamefutwa kazi baada ya mkanda wa video kuonesha mmoja wao akimkaba koo na goti lake raia mweusi, ambaye alifariki hospitalini Mei 26, 2020. Mtu ambaye hakuwa na silaha yoyote. kerem yucel / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Maafisa wanne wa polisi katika jimbo la Minesota nchini Marekani, wamefutwa kazi kufuatia kifo cha mwanamume mmoja, Mmarekani mweusi ambaye mkanda wa video umeonesha akikanyagwa shingoni hadi kupoteza maisha.

Matangazo ya kibiashara

Mkanda wa video umemwonesha mwanamume huyo mweusi kwa jina la George Floyd mwenye umri wa miaka 46, akimlalamikia polisi mzungu kuwa hawezi kupumua, huku akiwa amekanyagwa shingoni.

Tukio hili limelaaniwa na kuwakumbusha wengi tukio lingine kama hili, lilitokea katika mji wa New York mwaka 2014.

Meya wa mji wa Minnesota Jacob Frey amethibitisha kuwafuta kazi, maafisa hao wa polisi na kusema kitendo hicho hakikubaliki.

Maafisa wa Polisi nchini Marekani wameendelea kushtumiwa kwa kuwanyanyasa Wamarekani weusi katika miaka ya hivi karibuni, huku wengi wakikumbuka hivi majuzi, tukio la polisi kumpiga risasi na kumuua mwanamume mweusi ndani ya gari lake katika mji wa Maryland.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.