Pata taarifa kuu
MAREKANI-TWITTER-TRUMP-SIASA-USALAMA

Mtandao wa Twitter wakosoa ujumbe wa tweet wa rais wa Marekani Donald Trump

Rais Donald Trump katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, Mei 26, 2020.
Rais Donald Trump katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, Mei 26, 2020. Win McNamee/Getty Images/AFP
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Mtandao wa Twitter umeonya juu ya habari za uwongo zilizotolewa kupitia ujumbe wa tweet kutoka kwa rais wa Marekani Donald Trump. Mtandao huu wa kijamii haujawahi hadi sasa kukosoa maelfu ya jumbe za tweet za Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

Ujumbe uliorekebishwa unahusu upigaji kura kwa njia ya posta, njia ya kupiga kura iliyowasilishwa na rais kama mfumo wa udanganyifu.

Hii ni mara ya kwanza mtandao wa Twitter kujaribu kukosoa baadhi ya jumbe za twitter za rais Donald Trump.

"Kura inapofanyika kwa njia ya posta, husababisha udanganyifu. Hatutaruhusu nchi yetu iangamiye na mfumo huu usiofaa, "amesema Donald Trump Jumanne alasiri wiki hii.

Rais wa Marekani alikuwa akirejelea taarifa iliyoandikwa Jumanne asubuhi kwenye ukurasa wake wa Twitter, ameripoti mwandishi wetu huko Washington, Anne Corpet.

Lakini mstari mdogo wa bluu uliotanguliwa na alama ya mshangao ulionekana chini ya ujumbe wa tweet wa rais Donald Trump: "Angalia ukweli jkuhusu kupiga kura kwa njia ya posta. Kiunga kinasababisha maelezo haya: "Trump atahadharisha kwa mambo yasiyokuwa na msingi kuhusu zoezi la upigaji kura kwa nji aya posta. Hakuna ushahidi kwamba njia hii ya kupiga kura itasababisha udanganyifu. "

"Sitakubali jambo hili litokee!"

Kwa upande wake rais Trump ametaja hatua hiyo kama mojawapo ya kuminya uhuru wa kusema, akilaumu Twitter kwa kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani ambao unatazamiwa kufanyika Novemba mwaka huu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.