Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAUAJI-HAKI

Maandamano yashuhudiwa katika miji mbalimbali Marekani kulaani kuuawa kwa mwanaume mweusi

Maafisa wanne wa polisi kutoka Minneapolis chini Marekani walifutwa kazi baada ya video kuonesha mwanaume mweusi akikanyagwa shingoni na polisi mzungu, Mei 26, 2020.
Maafisa wanne wa polisi kutoka Minneapolis chini Marekani walifutwa kazi baada ya video kuonesha mwanaume mweusi akikanyagwa shingoni na polisi mzungu, Mei 26, 2020. kerem yucel / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Miji mbalimbali nchini Marekani imeshuhidia maandamano ya hasira kulaani kuuawa kwa mwanaume mweusi George Floyd, wiki hii katika jimbo la Minnesota, baada ya kukanyagwa shingoni na polisi mzungu.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji wenye hasira wameonekana wakiwasha moto barabarani na wengine kuvunja maduka katika mji wa Minneapolis.

Hasira ya umma inatokana na video iliyorikodiwa na mpita njia siku ya Jumatatu ikionesha polisi mzungu akitumia goti kumkandamiza shingoni mwanaume mmoja mweusi aliyefungwa pingu huku akiomba msaada kutokana na kukosa pumzi.

Floyd ambaye hakuwa na silaha lakini akituhumiwa kutaka kutumia fedha bandia kwenye mgahawa mmoja , alichukuliwa na gari ya wagonjwa kutoka eneo la mkasa huo na baadaye kufariki dunia.

Gavana wa jimbo la Minnesota Tim Walz ambaye amelitaka jeshi la akiba kuzuia kuharibiwa kwa maeneo ya biashara, hata hivyo amesema anawaelewa waandamanaji.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.