Pata taarifa kuu

Trump asaini sheria inayolenga mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter na Facebook

Donald Trump amesaini sheria inayolenga kudhibiti mitandao ya kijamii Alhamisi hii, Mei 28, katika Ikulu ya White House.
Donald Trump amesaini sheria inayolenga kudhibiti mitandao ya kijamii Alhamisi hii, Mei 28, katika Ikulu ya White House. REUTERS/Jonathan Ernst
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Rais wa Marekani Donald Trump amesaini sheria ambayo inalenga  kudhibiti mitandao ya kijamii. Hatua hii inakuja siku chache baada ya mtandao wa Twitter siku ya Jumanne kutaja jumbe mbili za Trump kuwa za kupotosha.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inajiri baada ya Trump kuukashifu Mtandao wa Twitter kwa kutaja chapisho lake kuwa potovu  ingawaje Trump hajatoa maelezo zaidi ya kuidhinisha sheria hiyo.

Mzozo huo uliibuka Jumanne wakati Mtandao wa Twitter ulihakiki ukweli wa baadhi ya ujumbe wa Rais wa Marekani Donald Trump alioundika katika ukurasa wake. Ni mara ya kwanza mtandao huo ambao Trump anapendelea zaidi kuutumia unafanya hivyo.

Rais wa Marekani alighadhibishwa na jambo hilo na kushumu mtandao huo kwa kile alichokiita ‘kuingilia kati' uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba pamoja na uhuru wa kujieleza.

Twitter ilichukua hatua hiyo ambayo haraka ilichochea mvutano kati yake na Trump, baada ya rais huyo wa Marekani kuandika Tweet mbili akidai kwamba mtindo wa kupiga kura kwa njia ya posta huwa una udanganyifu mwingi.

Ilichofanya Twitter ni kuweka kiungo kingine chini ya ujumbe wa Trump kinachosema "Pata taarifa za ukweli juu ya kura ya njia ya posta,” na baadae kiungo hicho kinampeleka mtumiaji kwenye makala ya habari inayompa taarifa za ukweli kuhusu suala hilo, na orodha ya maelezo yanayopinga madai ya Trump.

Trump mwenye wafuasi wapatao milioni 80 katika ukurasa wake wa Twitter, anasema anautumia mtandao huo wa kijamii kupinga kile anachodai kuwa ni taarifa za upendeleo zinazotolewa na vyombo vya habari.

Trump amekuwa akidai kwamba mtindo wa kupiga kura kwa njia ya posta, una viwango vya juu vya udanganyifu katika wakati ambapo majimbo mengi yanazingatia kuitumia njia hiyo ili kulinda afya ya raia dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 wakati taifa hilo likiwa linaelekea katika uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.