MAREKANI-MAUAJI-HAKI

Kifo cha George Floyd chaendelea kuzua sintofahamu Minneapolis, mhusika mkuu akamatwa

Maafisa wanne wa polisi kutoka Minneapolis chini Marekani walifutwa kazi baada ya video kuonesha mwanaume mweusi akikanyagwa shingoni na polisi mzungu, Mei 26, 2020.
Maafisa wanne wa polisi kutoka Minneapolis chini Marekani walifutwa kazi baada ya video kuonesha mwanaume mweusi akikanyagwa shingoni na polisi mzungu, Mei 26, 2020. kerem yucel / AFP

Sheria ya kutotoka nje usiku imetangazwa tangu Ijumaa, Mei 29, huko Minneapolis, nchini Marekani, ambapo afisa wa polisi alihusika katika kifo cha George Floyd, Mmarekani mweusi ambaye kifo chake kimezua maumivu ya kibaguzi nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Derek Chauvin, afisa wa polisi mzungu ambae alichukuliwa video, ikionesha kambana kwa kutumia goti shingoni, George Floyd kwa karibu dakika tisa, ameshitakiwa kwa kusababisha kifo pasipo kukusudia na mauwaji kwa kizembe.

Kifo cha George Floyd kilisababisha maamndamano makubwa katika miji mbalimbali nchini Marekani hasa katika mji wa Minneapolis.

Hata hivyo hali ya utulivu imerejea katika mji wa Minneapolis. Licha ya makabiliano ya mara kwa mara na matukio kadhaa, hali hiyo haina uhusiano wowote na hasira ambayo ilishuhudiwa hapo awali, hata kama wanaharakati wengine wanaendelea kutoa wito wa maandamano yenye vurugu, ameripoti mwandishi wetu maalum huko Minneapolis, Eric de Salve.

Maandamano ya siku kadhaa katika mji wa Minnesota yamesababisha uharibufu wa mali na kuchoma moto majumba ambayo pia yamesambaa katika maeneo mengine nchini Marekani.

Tukio hilo limesababisha hasira na ghadhabu nchini humo juu ya matukio mengine kama hayo ambapo polisi huwaua raia weusi wasiokuwa na hatia.

Habari za kukamatwa kwa kushitakiwa kwa askari huyo zimetolewa muda mfupi baada ya Gavana wa Jimbo Minnesota Tim Walz kuwataka wananchi kuachana na maandamano kwa ahadi ya kupatikana kwa haki katika kesi hiyo mpya.