UJERUMANI-MAREKANI-G7-USHIRIKIANO

Merkel akataa kuhudhuria mkutano wa G7 Washington

Rais wa Marekani, Donald Trump na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel katika mkutano wapamoja na waandishi wa habari jijini Washington Machi 17, 2017.
Rais wa Marekani, Donald Trump na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel katika mkutano wapamoja na waandishi wa habari jijini Washington Machi 17, 2017. REUTERS/Jim Bourg

Kansela Angela Merkel amekataa kuhudhuria mkutano wa kilele wa kundi la nchi 7 zenye uchumi wa juu zaidi duniani, G7, nchini Marekani mnamo mwezi Juni, kama ilivyopendekezwa na rais wa Marekani, Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

Angela Merkel amesema hatohodhuria mkutano huo, kwa sababu ya janga la Corona, msemaji wa serikali ya Ujerumani amelithibitishia shirika la habari la AFP leo Jumamosi.

"Kwa leo, ukizingatia hali ya jumla ya janga la Corona, hawezi kukubali kusafari kwenda Washington," amesema msemaji wa serikali ya Ujerumani, akithibitisha habari ya chombo cha habari mtandaoni cha Politico kutoka Marekani.

"Ofisi ya kansela aw Ujerumani inamshukuru rais Trump kwa mwaliko wake kwenye mkutano wa G7," msemaji wa serikali ya Ujerumani ameongeza.

Bi Merkel, ndiye kiongozi wa kwanza wa kundi la G7 (Japan, Canada, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia) kukataa rasmi mwaliko huu.

Umri wa Merkel, 65, ambaye pia ni sawa na ule wa Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, unamweka katika hatari kubwa ya kuambukizwa haraka janga la Covid-19.

Marekani ni nchi ya kwanza kuathirika zaidi duniani (zaidi ya watu 100,000 wamefariki dunia kwa Covid-19, huku watu Milioni 1.7 wakithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo).

Ikulu ya White ilikuwa imetangaza mwanzoni mwa mwezi Machi kuwa inasitisha maamdalizi ya mkutano huo, kwa sababu ya janga la Corona, kwa kuwaleta pamoja marais na viongozi wa serikali kutoka n-kundi la G7, ingependeleamkutano huo ufanyike kupitia video.

Lakini wiki iliyopita, Donald Trump alitangaza kwamba mkutano wa kilele wa kundi la G7 utafanyika mwezi wa Juni "katika Ikulu ya White House", ingawa kuna mikutano kadhaa ambayo inaweza kufanyika katika makazi ya rais ya Camp David, katika jimbo jirani la Maryland.