Kifo cha George Floyd: China yalaani 'ugonjwa sugu' wa ubaguzi wa rangi Marekani
Imechapishwa:
Machafuko katika miji kadhaa ya Marekani ni ishara tosha ya "kuongezeka kwa matatizo ya ubaguzi wa rangi na ghasia nchini humo," msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian ameviambia vyombo vya habari nchini China.
Kauli hii ya China inakuja wakati waandamanaji wanaopinga ubaguzi kwa mara nyingine tena wameingia mitaani katika miji nchini Marekani siku ya Jumapili kupaza sauti zao za hasiradhidi yaukatiliwapolisi.
Wakati viongozi wa maeneo mbali mbali wakitoa wito kwa raia kuonesha hasira zao kwa njia ya uadilifu kuhusiana na kifo cha mtu mmoja mweusi ambaye hakuwa na silaha, amri ya kutotembea usiku iliwekwa katika miji kama Los Angeles, Houston na Minneapolis , ambayo imekuwa kitovu cha machafuko.
Maandamano yaliyokuwa yakiangaliwa kwa karibu zaidi yalitokea nje ya ofisi za serikali katika mji pacha wa Minneapolis wa St.Paul ambako maelfu kadhaa ya waandamanaji walijikusanya kabla ya kuandamana katika barabara kuu.
Ripoti ya Uchunguzi ya West Philadelphia, imesema kuwa magari ya polisi pia yalichomwa moto.
Wakati huo huo utawala wa rais Donald Trump uliwaita wanaoongoza maandamano hayo yaliyofanyika katika usiku wa siku tano kuwa ni magaidi wa ndani.
Hayo yanajiri wakati Wakili wa familia ya George Floyd, ambaye kifo chake kiliibua maandamano ya hasira kote nchini Marekani , amemshutumu afisa wa polisi kwa "kupanga mauaji".
Tukio la Floyd limeibua ghadhabu miongoni mwa Wamarekani juu ya mauaji yanayotekelezwa na polisi dhidi ya watu weusi.
Hii inafuatia kesi maarufu ya mauaji ya Michael Brown mjini Ferguson, Eric Garner mjini New York na kesi nyingine zilizowasilishwa mahakamani na vuguvugu linalojulikana kama Black Lives Matters.