Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAUAJI-MAANDAMANO-HAKI

Kifo cha George Floyd: Miji mbalimbali Marekani yaendelea kukumbwa na maandamano

Maelfu ya watu wakiandamana kupinga kifo cha George Floyd, aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi, Houston, Juni 2, 2020.
Maelfu ya watu wakiandamana kupinga kifo cha George Floyd, aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi, Houston, Juni 2, 2020. Mark Felix / AFP

Watu 60,000 wameandamana kwa siku ya nane mfululizo katika miji mbalimbali ya Marekani ikiwa ni pamoja na mji wa Houston kupinga kifo cha kwa George Floyd, Mmarekani mweusi aliyefariki mikononi mwa polisi wa Minneapolis.

Matangazo ya kibiashara

Wengi wa waandamanaji walikua wamevalia fulana zenye picha ya George Floyd zikiandikwa maneno aliyoyasema kwa mara ya mwisho, "I can’ t breathe [siwezi kupumua]".

Katika maamndamano hayo pia wameshiriki baadhi ya Wazungu kutoka jamii mbalimbali, kwa mujibu wa mwandishi wetu huko Houston, Thomas Harms.

"Imenishangaza sana, lakini pia nilijawa na hisia nyingi kuona watu wengi, watu wa rangi mbalimbali, watu kutoka jamii tofauti wakiungana kwa kupinga kifo cha mtu mweusi, kwa kweli mji wa Houston umeonesha umoja wao, " amesema kijana mmoja.

Baadhi ya viongozi na maafisa wakuu wa polisi katika mji wa Houston wameonekana wakishiriki maandamano hayo, huku baadhi ya maafisa wa polisi wakiunga mkono waandamanaji.

Wakati huo huo Gavana wa Minnesota Tim Walz na idara ya haki za binadamu ya Minnesota wametangaza kufungua malalamiko rasmi katika mkutano na waandishi habari jana jioni. Gavana na kamishna wa haki za binadamu Rebecca Lucero wamesema wana matumaini kufikia makubaliano na mji huo kubaini njia za muda mfupi kuangalia historia ya idara ya polisi ya ubaguzi wa rangi, na kutumia uchunguzi huo kupata suluhisho la muda mrefu kwa ajili ya mabadiliko ya mfumo.

Meya Bill de Blasio ameongeza muda wa amri ya kutotembea usiku mjini humo, akiisogeza kutoka saa 5 usiku siku moja kabla , lakini alikataa miito ya rais Donald Trump na gavana Andrew Cuomo kuleta kikosi cha walinzi wa taifa.

Waandamanaji wameamua kukiuka hatua ya kusalia ndani iliyowekwa katika miji mbalimbali.

Msemaji wa serikali amesema vikosi vilikuwa katika tahadhari ya juu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.