MAREKANI-MAUAJI-MAANDAMANO-HAKI

Kifo kingine cha raia mweusi chazusha mandamano Marekani

Waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi walikusanyika huko Atlanta baada ya kifo cha Rayshard Brooks, aliyepigwa risasi na afisa wa polisi wa mji huo, Juni 14, 2020.
Waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi walikusanyika huko Atlanta baada ya kifo cha Rayshard Brooks, aliyepigwa risasi na afisa wa polisi wa mji huo, Juni 14, 2020. REUTERS/Elijah Nouvelage

Waandamanaji wenye hasira wanaendelea kuingia mitaani wakipinga kifo cha Rayshard Brooks, raia mweusi aliyeuawa wakati wa ukaguzi wa polisi na wiki tatu baada ya kifo cha Georges Floyd huko Minneapolis.

Matangazo ya kibiashara

Kifo cha raia huyo mweusi huko Atlanta, Georgia, kimezusha ghadhabu na maandamano tena, pamoja na mjadala unaoendelea ulimwenguni kote wa kupinga ubaguzi wa rangi.

Kujiuzulu kwa mkuu wa polisi Jumamosi hakujatuliza hasira za waandamanaji.

Wakati huo huo idara ya polisi ya Atlanta imesema, imemfuta kazi polisi mmoja kutokana na kifo hicho.

Rayshard Brooks, mwenye umri wa miaka 27 alipigwa risasi siku ya Jumamosi, alipokataa kukamatwa baada ya kufeli katika vipimo vya kubaini hali yake au ikiwa ametumia mihadarati.

Hayo yanajiri wakati maandamano yamekuwa yakiendelea nchini Marekani na kwingineko duniani kupinga kifo cha George Floyd aliyefariki dunia mwezi uliopita akiwa mikononi mwa polisi huko Minneapolis.