MAEKANI-CHINA-BOLTON-TRUMP-USALAMA-SIASA

Bolton amshutumu Trump kwa kutafuta msaada wa China ili aweza kuchaguliwa tena

Aliyekuwa mshauri wa rais wa Marekani Donald Trump kuhusu usalama wa kitaifa John Bolton.
Aliyekuwa mshauri wa rais wa Marekani Donald Trump kuhusu usalama wa kitaifa John Bolton. REUTERS/Joshua Roberts

Mshauri wa zamani wa rais wa Marekani Donald Trump kuhusu usalama wa kitaifa, John Bolton amemshutumu rais Trump kwa kutafuta msaada kutoka China ili aweze kushinda uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na kitabu John Bolton alichoandika na ambacho ikulu ya Marekani imeshitaki kutaka kisizinduliwe, rais Donadl Trump alimtaka kiongozi wa China Xi Jinping kumsaidia ili achaguliwe tena katika muhula wa pili kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka huu.

John Bolton amesema kwamba mwezi Juni 2019, Donald Trump "aligeuza mazungumzo kuhusu uchaguzi ujao wa urais, kwa kuzingatia uwezo wa kiuchumi wa China na kwa kumrai rais wa China Xi Jinping kumsaidia ili aweze kushinda katika uchaguzi huo”, kulingana na baadhi ya maneneo yaliyochapishwa na Magazeti ya Wall Street, New York Times na Washington Post.

Wakati wa mkutano huu kando ya mkutano wa kilele wa G20 huko Osaka, rais wa Marekani "alisisitiza umuhimu wa wakulima na kuongezeka kwa ununuzi wa bidhaa kutoka China hususan soya na ngano ikiwa atachaguliwa tena kwa muhula wa pili kuwa rais wa Marekani", ameandika kwenye kitabu chake.

Bolton amedai kuwa nia ya Trump kutaka kuchaguliwa tena ndiyo imekuwa msingi wa sera yake ya mambo ya kigeni.

Kitabu hicho kinachoitwa “The Room Where it Happened” yaani Chumba ambacho kilitokea’ kinatarajiwa kuzinduliwa Jumanne ya wiki ijayo.