BRAZILI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Karibu kesi 40,000 za maambukizi zathibitishwa Brazili

Serikali ya Brazili imethibitisha vifo vipya 1,141 na kufanya jumla ya watu 54,971 waliofariki dunia nchini Brazili kwa sababu ya janga hilo.
Serikali ya Brazili imethibitisha vifo vipya 1,141 na kufanya jumla ya watu 54,971 waliofariki dunia nchini Brazili kwa sababu ya janga hilo. REUTERS/Ueslei Marcelino

Brazili imerekodi kesi mpya 39,483 za maambukizi ya viriusi vya Corona siku ya Alhamisi wiki hii, Wizara ya Afya ya Brazili imetangaza. Jumla ya watu Milioni 1 na Laki 2 na Elfu 30 wameambukizwa virusi hivyo. Wagonjwa laki 6 na Elfu 50 wamepona ugonjwa huo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla, zaidi ya kesi milioni 1.2 zimerekodiwa nchini Brazil tangu kuzuka janga la Covid-19.

Serikali ya Brazili imethibitisha vifo vipya 1,141 na kufanya jumla ya watu 54,971 waliofariki dunia nchini Brazili kwa sababu ya janga hilo.

Watalaam wa afya aidha wameonya kuwa nchi hiyo itandelea kushuhudia ongezeko la maambukizi katika siku zijazo.

Wakati hayo yakijiri mataifa kadhaa ya bara la Ulaya yanaendelea kurejea katika hali ya kawaida. Uhispania imefungua mipaka yake na nchi za Umoja wa Ulaya.

Wakati huo huo shirika la Afya duniani, linasema maambukizi ya virusi vya Corona yameongezeka kwa kipindi cha wiki moja iliyopita barani Ulaya, hali ambayo inazua wasiwasi wa kuendelea kushuhudiwa kwa maambukizi mapya.

WHO inasema hatua za makusudi zinastahili kuchukuliwa kudhibiti hali hii ili kuepusha mataifa ya bara hilo kulemewa na ongezeko la virusi hivyo, wakati huu mataifa mengi yanapoanza kurejea katika hali ya kawaida.