MIXICO-USALAMA

Mexico: Miili ya watu 14 yagunduliwa barabarani Kaskazini mwa Mexico

Wataalam wanasema angalau makundi matatu ya uhalifu katika eneo hilo yenye uhusiano na makundi makubwa ya Sinaloa na "Jalisco New Generation" yamekuwa yakipigania udhibiti wa eneo la Zacatecas.
Wataalam wanasema angalau makundi matatu ya uhalifu katika eneo hilo yenye uhusiano na makundi makubwa ya Sinaloa na "Jalisco New Generation" yamekuwa yakipigania udhibiti wa eneo la Zacatecas. ©USA Today

Tangu mwaka 2006, Mexico imepeleka jeshi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ili kukabiliana na uhalifu unaoendelea nchini humo. 'Vita dhidi ya madawa ya kulevya' pia imesababisha wimbi kubwa la machafuko nchini, karibu watu 290,000 wameuawa tangu tarehe hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Miili kumi na minne iligunduliwa kwenye barabara kaskazini mwa mji wa Mexico, ambapo kunaripotiwa makundi ya wahalifu, maafisa wa eneo hilo wamesema.

"Upande wa ofisi ya mashtaka imethibitisha kwamba miili iliyogunduliwa asubuhi ya leo ni 14 ," serikali ya jimbo la Zacatecas imesema katika taarifa. Madreva ndio wameanza kuona miili hiyo ambayo ilikuwa imehifadhiwa kwenye blanketi kwenye barabara ya wilaya ya Fresnillo.

Kulingana na mwendesha mashtaka wa eneo hilo, Florida Murillo, miili minne tayari imetambuliwa. Ni wanaume wanne kutoka eneo ambalo liko kilomita 150 kutoka Fresnillo na "wameripotiwa kutoweka siku chache zilizopita".

Jimbo la Zacatecas liko kwenye moja ya barabara kuu kunakosafirishwa madawa ya kulevya kwenda Marekani. Wataalam wanasema angalau makundi matatu ya uhalifu katika eneo hilo yenye uhusiano na makundi makubwa ya Sinaloa na "Jalisco New Generation" yamekuwa yakipigania udhibiti wa eneo hilo.

Licha ya kuendelea kwa ugonjwa hatari wa Corona huko Mexico, machafuko bado yanaendelea. Siku ya Jumatano, watu kumi na sita waliuawa katika mapigano kati ya makundi hasimu ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya huko Tepuche, jamii ya vijijini katika jimbo la Mexico la Sinaloa (kaskazini mashariki).

Siku ya Ijumaa, mkuu wa usalama katika mji mkuu Mexico, Omar Garcia Harfuch alijeruhiwa kwa risasi katika shambulio lililohusishwa makundi ya wafanyabiasha wa madawa ya kulevya, shambulio ambalo liligharimu maisha ya watu watatu.