MIXICO-USALAMA

Mkuu wa polisi wa mji wa Mexico aponea kuuawa

Mkuu wa usalama wa mji mkuu wa Mexico, Omar Harfuch Garcia alishambuliwa alfajiri Ijumaa, Juni 26 katika mji wa Mexico.
Mkuu wa usalama wa mji mkuu wa Mexico, Omar Harfuch Garcia alishambuliwa alfajiri Ijumaa, Juni 26 katika mji wa Mexico. REUTERS/Henry Romero

Mkuu wa polisi wa mji wa Mexico amejeruhiwa wakati wa jaribio la kumuua, tukio lililotokea Ijumaa wiki hii. Gari yake ilishambuliwa na kundi la watu 28 waliokuwa wamejihami kwa silaha za kivita.

Matangazo ya kibiashara

Wakati wa shambulio hilo, Omar Harfuch Garcia, alifanikiwa kukimbia lakini alijeruhiwa kwa risasi tatu. Kundi la wafanyabiashara ya madawa ya kulevya la Jalisco linahusishwa katika shambulio hilo.

Mexico kwa miezi kadhaa ilikuwa haijashuhudia mashambulizi mabaya kama hayo. Shambulio hilo linatoa ujumbe kwa viongozi kwamba kila mtu atafikiwa.

Omar Harfuch Garcia, alishambuliwa katika kitongoji cha Lomas de Chapultepec, ambapo kunapatikana balozi kadhaa za nchi za kigeni. Walinzi wake wawili walipoteza maisha katika shambulio hilo.V

Saa chache baadaye, Omar Harfuch, kwenye mtandao wa Twitter alilishtumu kundi la wafanyabiashara wa madawa ya kulrvya la Jalisco Nueva Generacion kuhusika na shambulio hilo.