VENEZUELA-EU-USHIRIKIANO

Venezuela: Rais Maduro amtimua balozi wa Umoja wa Ulaya

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, ameuomba Umoja wa Ulaya kutoingilia masuala ya ndani ya nchi yake.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, ameuomba Umoja wa Ulaya kutoingilia masuala ya ndani ya nchi yake. REUTERS/Fausto Torrealba

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametoa muda wa saa 72 kwa balozi wa Umoja wa Ulaya awe ameondoka katika ardhi ya Venezula kabla hatua kali hazijachukuliwa, vyombo vya habari nchini humo vimebaini.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo inakuja baada ya Umoja wa Ulaya, EU, kuchukulia vikwazo kundi la wawakilishi wa Venezuela kwa hatua zao dhidi ya baraza la Congress ambapo upinzani una viti vingi.

Wakati huo huo Umoja aw Ulaya umelaani hatu hiyo ya kufukuzwa kwa balozi wake nchini Venezuela.

Mkuu wa sera ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amelaani hatua hiyo ya rais wa Venezuela na kutangaza hatua za "kukabiliana" na uamuzi huo.

"Tunalaani na tunafutilia mbali hatua hiyo ya kufukuzwa kwa balozi wetu huko Caracas na tutachukua hatua za kukabiliana na uamuzi huo," Josep Borrell amesema katika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter.