MAREKANI-TRUMP-BIDEN-SIASA-USALAMA

Maafisa katika utawala wa George W. Bush kumuunga mkono Biden dhidi ya Trump

Mgombea wa urais wa kutoka chama cha Democratic, Joe Biden, katika mkutano na waandishi wa habari Juni 30, 2020 huko Wilmington, Delaware.
Mgombea wa urais wa kutoka chama cha Democratic, Joe Biden, katika mkutano na waandishi wa habari Juni 30, 2020 huko Wilmington, Delaware. ALEX WONG / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / Getty Images via AFP

Mamia ya maafisa wa zamani serikalini ambao walifanya kazi katika utawala wa George W. Bush kutoka Chama cha Republican najiandaa kumuunga mkono Joe Biden kutoka chama cha Democratic, mshindani wa Donald Trump katika uchaguzi wa rais wa Novemba 3, vyanzo kadhaa vimebaini.

Matangazo ya kibiashara

Mawaziri na maafisa wakuu wa zamani katika utawala wa Bush (2001-2009) ni miongoni mwa wajumbe wa kundi hili, ambalo linaundwa kama kamati ya hatua ya kisiasa, iliyoitwa "Alumni 43 for Biden" (Maafisa wa zamani katika jamhuri ya 43 wanamuunga mkono Biden). George W. Bush alikuwa rais wa 43 wa Marekani.

Mpango huo utawekwa wazi katika saa zijazo, pamoja na uzinduzi wa tovuti na ukurasa wa Facebook.

Lengo ni kurusha hewani "ushuhuda wa video" kwa niaba ya Joe Biden na kujihusisha katika uhamasishaji wa uchaguzi katika majimbo muhimu "Swing States", ambayo ndio yanampa ushindi rais kulingana na matokeo ya uchaguzi, ikiwa imesalia zaidi ya miezi minne sasa kabla ya uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa sheria inayosimamia shughuli za kamati za hatua za kisiasa, au Super PAC, wajumbe wa Alumni 43 hawataweza kufanya kazi au kujadili na timu ya kampeni ya Joe Biden lakini wataweza kuongeza fedha bila kujali kiwango kwa kufadhili kampeni za matangazo au kuandaa maandamano ya kuunga mkono.

"Tunajua kinachokaa sawa, na kile kile ambacho hakijakaa, na tunachokiona kwa sasa hakijakaa sawa," amesema Jennifer Millikin, mmoja wa maafisa wa zamani wa timu ya kampeni ya uchaguzi ya Bush wakati alichaguliwa tena mnamo mwaka 2004 na mjumbe wa zamani wa usimamizi mkuu wa huduma ambaye ni mmoja wa waandaaji wa kundi la 43 Alumni.

Wafuasi wengine kutoka chama cha Republican tayari wameonyesha upinzani wao kwa kuchaguliwa tena Donald Trump, ishara kwamba rais ametengwa na sehemu ya watu katika chama chake.

Na usimamizi wake katika kudhibiti janga la Corona, kauli zake dhidi ya waandamanaji wenye hasira na kupinga dhidi ya ukatili wa polisi na ukosefu wa haki kwa ubaguzi wa rangi dhidi ya jamii ya watu weusi, yote hayo yamezidisha hali hiyo.

"Mnamo mwezi Novemba, tutachagua viongozi bora watakaoendeleza nchi yetu kuliko chama chetu," amesema, Kristopher Purcell, ambaye alifanya kazi katika sekta ya mawasiliano katika ikulu ya White House chini ya utawala wa George W. Bush, huku akibaini "Tunaamini kuwa serikali ya Biden itaheshimu utawala wa sheria na kurudisha hadhi na uadilifu wa Ikulu ya White House."