BRAZILI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo yapindukia zaidi ya 60,000 Brazil

Brazil inakuwa nchi ya pili kuathirika zaidi na duniani baada ya Marekani.
Brazil inakuwa nchi ya pili kuathirika zaidi na duniani baada ya Marekani. NELSON ALMEIDA / AFP

Brazil imerekodi Jumatano wiki hii vifo zaidi ya 60,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona, baada ya kuthibitisha vifo vipya 1038 katika muda wa saa 24 zilizopita, Wizara ya Afya imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Brazil, ambayo ni nchi duniani ambapo hivi karibuni ugonjwa wa Covid-19 uliuwa watu wengi kwa vifo vya kila siku kwa karibu wiki moja, imerekodi jumla ya vifo 60,632, kulingana na takwimu za wizara hiyo, idadi ambayo inachukuliwa kuwa ni ndogo na jumuiya ya wanasayansi.

Kwa jumla, zaidi ya kesi milioni 1.2 zimerekodiwa nchini Brazil tangu kuzuka janga la Covid-19.

Watalaam wa afya aidha wameonya kuwa nchi hiyo itandelea kushuhudia ongezeko la maambukizi katika siku zijazo.