MEXICO-USALAMA

Ishirini na nne waangamia katika shambulio katikati mwa Mexico

Makundi ya uhalifu kama vile Jalisco Nueva Generacion cartel na Santa Rosa de Lima cartel yamendelea kuendesha vitendo viovu katika jimbo Guanajuato, ikiwa ni pamoja na vitendo vya wizi, utekaji nyara na wizi wa mafuta.
Makundi ya uhalifu kama vile Jalisco Nueva Generacion cartel na Santa Rosa de Lima cartel yamendelea kuendesha vitendo viovu katika jimbo Guanajuato, ikiwa ni pamoja na vitendo vya wizi, utekaji nyara na wizi wa mafuta. PEDRO PARDO / AFP

Watu ishirini na nne wameuawa katika shambulio lililotekelezwa na watu wenye silaha katika kituo tiba kwa ajili ya waathiriwa wa madawa ya kulevya huko Irapuato, katika jimbo la Guanajuato, kulingana na mamlaka katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

"Watu waliojihami kwa silaha waliwasili kwa gari nyekundu, na mpaka sasa hatuna maelezo zaidi. Kulingana na ripoti ya awali, watu 24 wameuawa na 7 wamejeruhiwa," mkuu wa idara ya usalama wa umma katika eneo la Irapuato, Pedro Cortés, amebaini.

Ripoti za awali zinaonyesha kuwa watu waliyojihami kwa bunduki walivamia kituo tiba kwa ajili ya waathiriwa wa madawa ya kulevya, na kuwalazimisha watu walale chini na kuwafyatulia risasi.

Mamlaka inatafuta gari ambayo iliswasafirisha wauaji hao.Jimbo la Guanajuato, ambalo ni moja wapo ya maeneo yenye viwandani vingi Mexico, likiwa hasa na viwanda vikubwa vya kutengeneza magari, limemeendelea kukabiliwa na mashambulizi ya hapa na pale.

Makundi ya uhalifu kama vile Jalisco Nueva Generacion cartel na Santa Rosa de Lima cartel yamendelea kuendesha vitendo viovu katika jimbo hili, ikiwa ni pamoja na vitendo vya wizi, utekaji nyara na wizi wa mafuta, pamoja na biashara ya madawa ya kulevya.