MAREKANI-CORONA-AFYA

Marekani yarekodi visa vipya elfu hamsini vya maambukizi

Marekani inaendelea kurekodi vifo zaidi kutokana na ugonjwa wa Corona.
Marekani inaendelea kurekodi vifo zaidi kutokana na ugonjwa wa Corona. REUTERS/Brendan McDermid

Marekani imeshuhudia ongezeko kubwa la maambukizi ya Corona kwa mara ya kwanza kwa siku moja, baada ya watu wengine Elfu 50 kuambukizwa katika majimbo mbalimbali.

Matangazo ya kibiashara

Majimbo yaliyoshuhudia ongezeko hili ni Carlifonia na Florida katika taifa hilo lenye visa zaidi ya maambukizi zaidi ya Milioni Mbili na Laki Saba.

Nalo Shirika la Afya Duniani, WHO, linaonya kuhusu ongezeko la maambukizi hayo duniani, kipindi hiki ambacho mataifa mbalimbali yanapoanza kufungua uchumi wake.

Hayo yanajiri wakati Afrika Kusini imeanza jaribio la kwanza la kliniki la chanjo ya Covid-19 barani Afrika. Chanjo hii iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford na tayari imeanza kufanyiwa majaribio kwa binadamu nchini Uingereza.

Hivi karibuni Umoja wa Ulaya, ambao mipaka yake ya nje ilifungwa kama sehemu ya kupambana dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, ilifungua tena mipaka yao kuanzia Julai 1 kwa raia kutoka nchi 14 ambazo hali yao ya ugonjwa huchukuliwa kuwa ya kuridhisha, huku Marekani ikiwa haimo kwenye orodha hiyo.