MAREKANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya zaidi ya 57,000 vya maambukizi vyathibitishwa Marekani

Rais  wa  Marekani Donald Trump ameendelea kupuuzia  ongezeko  hilo  la  maambukizi  mapya.
Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea kupuuzia ongezeko hilo la maambukizi mapya. REUTERS/Mike Segar

Marekani imerekodi visa vipya 57,683 vya maambukizi ya virusi vya Corona ndani ya muda wa saa 24 Ijumaa wiki hii, kulingana natakwimu za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, ambacho kimesemaa, idadi hiyo ni kiwango cha rekodi tangu kuzuka kwa janga hilo.

Matangazo ya kibiashara

Marekani pia imerekodi vifo vipya 728 vinavyohusiana na ugonjwa wa Covid-19 wakati ikisherehekea uhuru, kulingana na chanzo hicho hicho, na kufanya jumla ya vifo kufikia 129,405.

Kutokana na hali hiyo, Uingereza imelazimika kuwaweka wasafiri kutoka Marekani kwenye orodha mbaya.

Wakati Ulaya na sehemu nyingi za Asia kwa kiasi kikubwa zimeweza kudhibiti virusi hivyo vya corona , kwa kiasi kikubwa Uingereza inajitayarisha kufungua biashara zake, mikahawa na cinema, lakini nchini Marekani ugonjwa huo umewauwa karibu watu 130,000 huku kukiwa na ongezeko kubwa la kesi mpya za maambukizi ambapo mtaalamu wa ngazi ya juu wa magonjwa ya kuambukiza Anthony Fauci amesema "unaiweka nchi nzima katika hatari."

Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea kupuuzia ongezeko hilo la maambukizi mapya.

Lakini mtangulizi wake Barack Obama amewataka wananchi aw Marekani kujiweka "salama na kuwa wajanja."

Kufikia sasa Marekani imerekodi visa vya maambukizi Milioni 2.85 baada ya visa vipya 57,683 kuthibitishwa, na wagonjwa 865,000 wamepona ugonjwa huo hatari.