BRAZILI-CORONA-AFYA

Visa vya maambukizi vyapindukia zaidi ya Milioni 1.5 Brazil

Kwenye makaburi ya Recanto da Paz, huko Breves, kusini magharibi mwa kisiwa cha Marajo katika jimbo la Para, Brazil, Juni 7, 2020.
Kwenye makaburi ya Recanto da Paz, huko Breves, kusini magharibi mwa kisiwa cha Marajo katika jimbo la Para, Brazil, Juni 7, 2020. REUTERS/Ueslei Marcelino

Brazil imerekodi visa vipya 42.223 vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda aw saa 24 na kufanya idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo hatari kufikia 1,539,081 Ijumaa wiki hii tangu kuzuka kwa janga hilo, Wizara ya Afya imesema.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, vifo vipya 1,290 vimethibitishwa, na kusababisha jumla ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo hatari kufikia 63,174 nchini Brazili.

Kufikia sasa Marekani ndio inaoongoza kwa idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona, ambapo kufikia jana ilikuwa na wagonjwa Milioni 2.85.

Wakati huo huo Shirika la Afya Duniani, WHO, limeyataka mataifa ya Afrika ambayo yameanza huduma za safari za ndege kuweka masharti muhimu, yatakayosaidia kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya Corona.

WHO inataka taarifa za abiria kuchukuliwa na kufuatiliwa, wakati huu Cameroon, Equatorial Guinea, Tanzania na Zambia yakianza safari za angaa.

Maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika yamefikia zaidi ya Laki nne, huku watu wengine zaidi ya Elfu 10 wakipoteza maisha.