BRAZILI-CORONA-AFYA

Jair Bolsonaro: Sijaambukizwa virusi vya Corona, lakini ninaepuka kuwakaribia watu

Rais Bolsonaro ambaye mara kwa mara amekuwa akikataa kuvaa barakoa amesema pia amechunguzwa mapafu kwa kutumia kipimo cha picha cha X-ray katika hospitali ya kijeshi kama tahadhari.
Rais Bolsonaro ambaye mara kwa mara amekuwa akikataa kuvaa barakoa amesema pia amechunguzwa mapafu kwa kutumia kipimo cha picha cha X-ray katika hospitali ya kijeshi kama tahadhari. Sergio LIMA / AFP

Rais wa wa Brazili Brazil Jair Bolsonaro amesema amepimwa Corona na matokeo yake yamebaini hajaambukizwa, baada ya shirika moja la utangazaji kuripoti rais huyo alikuwa na dalili zinazofanana na za Corona.

Matangazo ya kibiashara

Rais Bolsonaro amekuwa akipuuzia mbali hatari ya Corona, na nchi yake sasa ni miongoni mwa mataifa yaliyoathirika mno, ikiwa imeripoti visa zaidi ya milioni moja na sita na vifo elfu 65.

Rais Bolsonaro ambaye mara kwa mara amekuwa akikataa kuvaa barakoa amesema pia amechunguzwa mapafu kwa kutumia kipimo cha picha cha X-ray katika hospitali ya kijeshi kama tahadhari.

Rais huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 65, amesema amekuwa akitumia dawa ya hydroxychloroquine, kama hatua za kujikinga. Vyombo vya habari vya Brazil vimetangaza kuwa Bolsonaro amebadili ratiba yake ya wiki nzima, ingawa wasaidizi wake hawajatoa taarifa yoyote.

Brazili inaendelea kushikilia nafasi ya pili kwa vifo zaidi duniani vinavyohusiana na janga la Covid-19 baada ya Marekani ambayo inaongoza kwa visa zaidi ya Milioni 2 vya maambukizi.

Brazili, ambayo ni nchi kubwa katika ukanda wa Amerika ya Kusini (yenye wakaazi milioni 212) pia ni ya pili kwa idadi kubwa ya maambukizi yaliyothibitishwa nyuma ya Marekani, ikiwa na visa 828,810 vya maambukizi, shirika la habari la AFP limeripoti.