MAREKANI-NEW YORK-CORONA-AFYA

New York yaweka majimbo matatu karantini

Marekani imeendelea kurekodi visa vingi vya maambukizi ya Corona na ni nchi ambayo inaoongoza kwa maambukizi duniani, ikifuata na Brazil.
Marekani imeendelea kurekodi visa vingi vya maambukizi ya Corona na ni nchi ambayo inaoongoza kwa maambukizi duniani, ikifuata na Brazil. REUTERS/Mike Segar

Gavana wa jimbo la New York ameagiza mamlaka katika jimbo hilo kuwaweka karantini raia kutoka majimbo matatu ambayo ni Delaware, Kansas na Oklahoma, baada ya majimbo hayo kurekodi visa vingi vya maambukizi ya virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Katika majimbo haya matatu, Gavana Andrew Cuomo amebaini kwamba, virusi vya SARS-CoV-2 vimeendelea kusambaa na kuwa na hofu kuwa huenda vikasambaa hadi katika jimbo lake, ikiwa hapatakuwa na hatua za kudhibiti maambukizi hayo.

Kwa jumla, Jimbo la New York limeanza kuwaweka karantini wasafiri kutoka majimbo 19 ya Marekani.

Marekani imeendelea kurekodi visa vingi vya maambukizi ya Corona na ni nchi ambayo inaoongoza kwa maambukizi duniani, ikifuata na Brazil.

Kufikia sasa Marekani imerekodi visa Milioni 2.99, baada ya visa vipya 46,727 kuthibitishwa, na vifo 132,000 baada ya vifo vipya 244 kuthibitishwa katika muda wa saa 24. Wagonjwa 901,000 wamepona ugonjwa huo nchini Marekani