MAREKANI-UCHUMI-HAKI

Mahakama Kuu kutoa uamuzi wake kuhusu kukataa kwa Trump kutangaza mali yake

Mmoja wa waandamanaji akibebelea bango lililoandikwa "Fuata pesa hizo" mbele ya Mahakama Kuu ya Marekani, Juni 30, 2020 huko Washington.
Mmoja wa waandamanaji akibebelea bango lililoandikwa "Fuata pesa hizo" mbele ya Mahakama Kuu ya Marekani, Juni 30, 2020 huko Washington. AFP

Mahakama Kuu ya Marekani inatarajia kutoa uamuzi wake Alhamisi hii katika kesi inayohusiana na mali ya Donald Trump na kinga ya rais inayomlinda.

Matangazo ya kibiashara

Jumatano wiki hii Korti ya juu zaidi nchini Marekani imesema kuwa itatoa maamuzi yake ya mwisho ya kipindi cha mwaka 2019-2020, ambapo maamuzi mawili yanamuhusu rais Donald Trump kutoka chama cha Republican.

Rais Donald Trump anapinga kuwasilishwa kwa hati zinazohusiana na mali yake, jambo ambalo liliombwa na kamati ya bunge na mwendesha mashtaka wa Jimbo la New York.

Suala la kwanza katika faili hii liko wazi: uamuzi wa Mahakama Kuu unaweza kusaidia kuondoa mashaka kabla ya uchaguzi wa urais Novemba 3 kuhusu fedha za Donald Trump, ambaye ni tofauti na watangulizi wake wote tangu miaka ya 1970 amekataa kutangaza mali yake na aeleze jinsi alivyopata mali hiyo, na ushuru anaolipa kwa Serikali.

Suala la pili, la muda mrefu linahusu kinga ya rais ambayo ananufaika nayo wakati bado yupo ikulu White House.

Kwa upande wa mawakili wake, wanasema inahitajika kumlinda kutokana na jaribio lolote la "unyanyasaji" ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa utulivu.