MAREKANI-TRUMP-CORONA-AFYA-SIASA

Trump ziarani Florida, ambapo janga la Covid-19 linavunja rekodi

Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea kupuuzia taarifa kwamba idadi ya maambukizi na vifo inaendelea kuongezeka nchini Marekani.
Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea kupuuzia taarifa kwamba idadi ya maambukizi na vifo inaendelea kuongezeka nchini Marekani. AFP

Rais wa Marekani, Donald Trump anasafiri kwenda Florida, moja wapo ya maeneo kunakoripotiwa idadi kubwa ya maambukizi ya Covid-19, kabla ya mkutano mpya wa kampeni za uchaguzi Jumamosi huko New Hampshire.

Matangazo ya kibiashara

Rais Trump ameuuzia onyo la kiafya na kusema kuwa ni uwongo rekodi za sasa za maambukizi zinazotolewa na mashirika mbalimbali na vyombo vya habari.

"Tumefanya vipimo kwa watu milioni 40 au 45, ni rekodi, na vipimo vyetu ni vizuri zaidi," alisema Donald Trump kwenye Fox News siku ya Alhamisi. "Kesi nyingi huimarika mara moja. Kweli watu wanaumwa lakini siku mbili baadaye wanakuwa sawa."

"Unapowasha televisheni, wanazungumza tu kila mara kuwa hali ni mbaya na idadi ya maambukizi inaendelea kuongezeka kila kukicha. Hawazungumzii juu ya vifo, kwa sababu idadi ya vifo imepungu mno," ameongeza.

Idadi ya vifo kutokana na Covid-19, nchini kote, imeshuka tangu mwezi wa Aprili baada ya hali kuimarika huko New York, lakini idadi ilianza tena kuongezeka, na watu kadhaa walioambukizwa mwezi Juni walianza kufariki mmpja baada ya mwengine.

Siku ya Alhamisi, Texas na Florida, kila jimbo, liliripoti rekodi yao ya vifo tangu kuzuka kwa janga hilo, ambapo Texas lilirekodi vifo 98, huku Florida ikiripoti vifo 120.

"Tsunami bado ipo," kiongozi wa serikali ya Kaunti ya Hidalgo, hukoTexas Kusini amesema. Kesi mpya 1,274 za mambukizi zimethibitishwa katika muda wa saa 24 katika eneo hili lenye wakazi 900,000.

Kwa kulinganisha, mji wa Australia wa Melbourne, wenye wakazi milioni 5, ulichukua hatua ya wakazi wake kutotembea baada ya kesi 191 za maambukizi kugunduliwa katika muda wa saa 24 wiki hii.