BRAZILI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo yapindukia zaidi ya 1,200 Brazil

Brazil ni nchi iliyoathiriwa zaidi na janga la Covid-19 duniani baada ya Marekani.
Brazil ni nchi iliyoathiriwa zaidi na janga la Covid-19 duniani baada ya Marekani. EVARISTO SA / AFP

Brazil imerekodi visa vipya 45,048 vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo vipya 1,214 vinavyohusiana na janga hilo katika muda wa saa 24 zilizopita, Wizara ya Afya imeripoti jana Ijumaa jioni.

Matangazo ya kibiashara

Idadi rasmi ya maambukizi katika nchi hii ya Amerika Kusini sasa imeongezeka hadi 1,800,827 na vifo 70,398.

Mapema wiki hii Rais wa Brazil Jair Bolsonaro alithibitishwa kuwa ameambukizwa virusi vya Corona, baada ya vipimo vinne ,vilivyochukuliwa baada ya rais huyo kuonesha dalili za Corona, ikiwemo joto jingi mwilini.

Rais Bolsonaro alinukukuliwa akipinga vikali kuwepo hatari ya ugonjwa huo na kugoma kutangaza kusitisha shughuli za kawaida akisema hatua hiyo ingeathiri mno uchumi.

Brazil ni nchi iliyoathiriwa zaidi na janga la Covid-19 duniani baada ya Marekani.