MAEKANI-TRUMP-UHAMIAJI-HAKI

Marekani: Rasimu ya sheria ya Trump kuhusu wahamiaji haitoi msamaha

Maandamano karibu na ikulu ya White House Septemba 5 dhidi ya uamuzi wa Donald Trump wa kusitisha kutoa hifadhi kwa wahamiaji haramu walioingia Marekani "Dreamers".
Maandamano karibu na ikulu ya White House Septemba 5 dhidi ya uamuzi wa Donald Trump wa kusitisha kutoa hifadhi kwa wahamiaji haramu walioingia Marekani "Dreamers". REUTERS/Aaron P. Bernstein

Rasimu ya sheria ya Rais Marekani Donald Trump kuhusu uhamiaji haitoi msamaha kwa wahamiaji ambao wapo nchini humo kinyume cha sheria lakini ambao waliingia nchini wakiwa watoto, msemaji wa ikulu ya White House amesema.

Matangazo ya kibiashara

"Hakuna msamaha kwa wahamiaji haramu," msemaji wa Ikulu ya White House amesema katika taarifa baada ya Trump kusema kwenye mahojiano ya Runinga kuwa muswada wake wa sheria hautawapa uraia wahamiaji hao wanaojulikana kwaa jina la "Dreamers".

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Uhispani cha Telemundo, Rais Trump amesema muswada wake wa sheria utahusu tu wahamiaji walioingia nchini Marekani wakiwa watoto (DACA), mpango ambao unalinda mamia ya maelfu ya wahamiaji hao kufukuzwa nchini Marekani.

Taarifa ya White House inasema agizo la Rais Trump litaanzisha mfumo wa uhamiaji unaojikita kwenye maadili mema na kwamba Trump anatarajia kushirikiana na Baraza la Congress juu kupatikana suluhisho la kisheria ambalo "linaweza kujumuisha uraia, na kudumoisha usalama dhabiti mipakani na mageuzi yenye sifa ya kudumu, "lakini hakuna msamaha.