BRAZILI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Brazil yaendelea kushuhudia ongezeko la maambukizi

Nchi za Brazil, India na Afrika Kusini zinaongoza katika kurekodi idadi ya juu kwa siku moja.
Nchi za Brazil, India na Afrika Kusini zinaongoza katika kurekodi idadi ya juu kwa siku moja. REUTERS/Ricardo Moraes

Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Brazil inakaribia milioni mbili. Hadi kufikia sasa nchi hii ina jumla ya visa zaidi ya Milioni moja kwa mujibu wa takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati shirika la afya duniani WHO likitangaza idadi ya maambukizi mapya kwa siku moja duniani ikivuka laki mbili na elfu 30, nchi za Brazil, India na Afrika Kusini zikiongoza katika kurekodi idadi ya juu kwa siku moja.

Wakati huo huo shirika la kutetea haki za watoto la Save the Children, limeonya kuwa huenda watoto milioni 10 wameathirika baada ya shule kufungwa kutokana na janga la Corona na huenda wasirejee tena shuleni.

Shirika hilo pia limesema huenda watoto kati ya milioni 90 na milioni 117 wakaishi katika hali ya umasikini kutokana na makali ya kiuchumu.