MAREKANI-CORONA-AFYA-SIASA

Coronavirus: Maambukizi zaidi yathibitishwa katika Jimbo la Florida, Marekani

Jimbo la Florida limevunja rekodi ya jimbo la New York ambalo liliwahi kuripoti visa zaidi ya Elfu 12, tarehe 10 mwezi Aprili.
Jimbo la Florida limevunja rekodi ya jimbo la New York ambalo liliwahi kuripoti visa zaidi ya Elfu 12, tarehe 10 mwezi Aprili. REUTERS/Lucas Jackson

Maambukizi ya virusi vya Corona duniani yanaendelea kuongezeka wakati huu jimbo la Florida nchini Marekani limeripoti maambukizi mapya Elfu 15 kwa muda wa saa 24 zilizopita, wakati huu serikali ya rais Donald Trump ikitaka shule kufunguliwa.

Matangazo ya kibiashara

Ongezeko hili la maambukizi katika jimbo la Floroda, linalifanya kuingia kwenye vitabu vya historia vya kuripoti idadi kubwa ya maambukizi kwa siku moja hata zaidi ya taifa lolote la bara Ulaya, ambalo maambukizi hayo yameanza kupungua.

Jimbo hilo limevunja rekodi ya jimbo la New York ambalo liliwahi kuripoti visa zaidi ya Elfu 12, tarehe 10 mwezi Aprili.

Hii inaifanya Marekani kuendelea kuongoza kwa maambukizi ya virusi vya Corona, ikiwa na visa zaidi ya Milioni tatu na kufuatwa na Brazil, huku India ikiwa katika nafasi ya tatu.

Wakati ongezeko hilo likiripitiwa, rais Donamld Trump ambaye majuzi kwa mara ya kwanza alivalia barakoa, ameendelea kuwahimiza Magavana wa majimbo mbalimbali kufungua majimbo yao ili kuokoa uchumi wa nchi hiyo, wakati huu taifa hilo likielekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba.